10.5 C
New York

Stars yang’olewa kibishi AFCON 2025

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeondoshwa kwenye fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) lakini gumzo ni penalti waliyonyimwa katika mchezo wao wa hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo dhidi ya Morocco.

Katika mechi hiyo ya leo Januari 4, 2025, Morocco waliitanguliza kuziona nyavu za Stars kupitia kwa Brahim Diaz aliyetumia ‘asisti’ ya Achraf Hakimi kufunga kwa shuti kali dakika ya 64.

Muda mfupi kabla ya bao hilo, Feisal Salum ‘Fei Toto’ angeweza kuifungia Stars lakini shuti lake lilipaa juu ya lango akiwa ndani ya boksi baada ya kufikiwa na mpira uliotemwa na kipa wa Morocco, Yassine Bounou.

Lakini, tukio lililowaibua mjadala mkubwa wakati na hata baada ya mchezo huo ni lile la mwamuzi wa kati, Boubou Traore, kuinyima Stars penalti ya wazi.

Mwamuzi huyo wa kimataifa wa Mali alifumbuia macho kitendo cha Iddy Suleiman ‘Nado’ wa Stars kuchezewa rafu ndani ya boksi, dakika chache kabla ya mchezo huo kumalizika.

Licha ya kuwapo kwa teknolojia ya VAR, Traore aligoma kwenda kupata msaada wa marudio ya video juu ya tukio hilo lililolalamikiwa na wachezaji na benchi la ufundi la Stars.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img