22 C
New York

Dereva wa Joshua ashitakiwa

Published:

LAGOS, Nigeria

DEREVA, Adeniyi Mobolaji Kayode (46) aliyekuwa akiendesha gari lililopata ajali iliyomjeruhi bondia wa uzito wa juu duniani, Anthony Joshua, amefunguliwa mashitaka.

Akiwa Nigeria kwa mapumziko hivi, Joshua alipata ajali iliyosababisha vifo vya watu wake wawili, kwa mujibu wa taarifa ya polisi.

Watu wake waliopoteza maisha siku hiyo ni kocha mkuu, Latif Ayodele, pamoja na msaidizi wake kwa upande wa mazoezi ya viungo, Sina Ghami.

Kayode, raia wa Nigeria, ambaye ndiye aliyekuwa dereva, amepandishwa kizimbani kwa makosa manne.

Kayode anashitakiwa kwa uzembe, mwendo mkali, pia akitajwa kutokuwa na leseni, kwa mujibu wa BBC.

Hata hivyo, dereva huyo ameachiwa kwa dhamana baada ya kulipa Pauni 2,578, na kesi yake itasikilizwa tena Januari 20, mwaka huu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img