18 C
New York

Endrick rasmi atua Lyon

Published:

MADRID, Hispania

KLABU ya Lyon ya Ligue 1 imethibitisha kukamilisha usajili wa mshambuliaji kinda wa Real Madrid, Endrick Felipe. Taarifa zinaeleza kuwa Lyon wamemchukua Mbrazil huyo kwa mkopo wa hadi mwishoni mwa msimu huu.

Endrick (19), alitua Santiago Bernabeu mwaka jana akitokea Palmeiras ya Ligi Kuu nchini Brazil.
Katika msimu wake wa kwanza, alicheza mechi 22 za Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) lakini akapoteza nafasi tangu Xabi Alonso alipoajiriwa kuinoa Madrid.

Sasa, amejiunga na Lyon ili kupata nafasi ya kucheza, ikielezwa kuwa klabu hiyo imeilipa Madrid kiasi cha euro milioni moja.
Mkataba wake utafikia ukomo Juni 30, mwakani, na anaikuta Lyon ikiwa nafasi ya tano katika msimamo wa Ligue 1.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img