LONDON, Uingereza
HUENDA kiungo wa pembeni wa Chelsea, Raheem Sterling, akaondoka klabuni hapo na kujiunga na Leeds United au Crystal Palace za Ligi Kuu ya England (EPL).
Sterling mwenye umri wa miaka 31, alikaribia kutimka Stamford Bridge wakati wa usajili uliopita wa majira ya kiangazi, mwaka huu.
Hivyo, kwa sasa ripoti zinaeleza kuwa winga huyo ataondoka Chelsea wakati wa dirisha dogo la Januari, mwakani.
Sterling, licha ya kutakiwa Serie A na Saudi Arabia, amekuwa akisisitiza juu ya mpango wake wa kubaki jijini London hata kama atatimka Chelsea.
Leeds inataka kumsajili ikiamini ni mchezaji muhimu katika kuimarisha mapambano yao ya kubaki Ligi Kuu ya England kwa msimu ujao.
Chini ya kocha Daniel Farke, timu hiyo haijafungwa katika mechi tatu ilizocheza hivi karibuni, licha ya kukutana na Chelsea, Liverpool na Brentford.


