25.9 C
New York

Jeshi la Polisi lathibitisha kumshikilia Waziri wa zamani

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha  kuwa  linamshikilia Waziri wa zamani, Geoffrey Mwambe, kwa tuhuma za  jinai ambayo jeshi hilo limesema linachunguza.

‎Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Kanda maalum ya Polisi, leo Desemba 12, 2025, Mwambe alikamatwa Desemba 7, 2025, katika eneo la Tegeta Kinondoni.


Taarifa hiyo ya Polisi imekuja baada ya Wakili wa Mwambe, Hekima Mwasipu kuiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa amri ya kupewa dhamana au kufikishwa mahakamani kwa mteja wake katika maombi yenye namba 289778 ya mwaka 2025.

Mwambe aliwahi kuwa Mbunge wa Masasi, Mtwara kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), pia Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara na Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC).

Aidha, taarifa hiyo imebainisha kuwa, hali ya usalama jijini Dar es salaam ni nzuri na Wananchi wanaendelea na shughuli zao mbalimbali halali.

Related articles

Recent articles