5.7 C
New York

JKT Queens kuweka kambi Uturuki, yautaka ubingwa wa CAFWCL

Published:

Na Winfrida Mtoi, Gazetini

Timu ya soka JKT Queens inatarajia kuweka kambi ya wiki mbili  jijini  Istanbul, Uturuki kujiandaa na  michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake(CAFWCL), itakayofanyika  mwezi ujao  nchini Algeria.

Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisa Habari wa JKT Queens, Masau Bwire, timu hiyo ambayo tayari imeanza kambi, itaondoka nchini Oktoba 9, 2025 na sababu ya kuweka kambi Uturuki ni kuwaandaa wachezaji na hali ya hewa na Algeria ambayo inaendana na iliyopo Istanbul.

Ameeleza kuwa wakiwa huko wanatarajia kucheza mechi mbili za kirafiki  kwa ajili ya maandalizi hayo kutokana na ukumbwa wa mashindano hayo na malengo waliyojiwekea ambayo ni kuchukua ubingwa.

Ofisa Habari wa JKT Queens, Masau Bwire akizungumza na waandishi wa habari.

“Tunalenga ubingwa wa mashindano hayo ili kuleta heshima kwa Taifa na Ukanda wa CECAFA kwa kuwa JKT Queens ndiyo timu pekee inayowakilisha Ukanda huo. amesema Bwire.

JKT Queens ilipata nafasi ya kushiriki michuano hiyo baada ya kutwaa ubingwa wa Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Hii ni mara ya pili kwa timu hiyo kushiriki mashindano hayo makubwa ya Afrika  kwa wanawake ambapo kwa mara ya kwanza walishiriki 2023, nchini Ivory Coast.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img