25.3 C
New York

Wananchi wachoma Bunge, Waziri Mkuu ajiuzulu

Published:

KATHMANDU, Nepal
MAANDAMANO ya wananchi wenye hasira kali yamepelekea kuchomwa kwa ofisi za Bunge nchini Nepal, hatua iliyosababisha Waziri Mkuu kujiuzulu.
Hasira za wananchi zimetokana na madai ya Serikali yao kugubikwa na vitendo vya rushwa.
Waziri Mkuu, Sharma Oli, ametangaza kuachia ngazi wakati huu Nepal ikikabiliwa na maandamano ya kupinga mauaji ya raia 19 yaliyofanyika Jumatatu ya wiki hii.
Mbali ya kuchoma Bunge, pia wananchi walivamia na kuzifanyia uharibifu mkubwa nyumba za Serikali na zile za wanasiasa mbalimbali nchini humo.
Kutokana na maandamano hayo, watu watatu walipoteza maisha, hivyo kufanya idadi kufikia 21 tangu Jumatatu.
Aidha, kasi ya maandamano imeongezeka mara dufu baada ya hatua ya Serikali kufungia upatikanaji wa mitandao ya kijamii.
Wakati huo huo, wafungwa 900 wamejinufaisha na maandamano hayo kwa kutoroka katika magereza mawili ya Magharibi mwa Nepal.

Related articles

Recent articles