PARIS, Ufaransa
RAIS wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amemtangaza Sebastien Lecornu kuwa Waziri Mkuu mpya akichukua nafasi ya Francois Bayrou.
Lecornu mwenye umri wa miaka 39, alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kukalia kiti hicho tangu Bunge lilipopiga kura ya kutokuwa na imani na Bayrou.
Kabla ya uteuzi huo, Lecornu alikuwa Waziri wa Ulinzi kwa miaka mitatu ya hivi karibuni.
Ikumbukwe, Lecornu anakuwa Waziri Mkuu wa tano tangu Macron aliporejea madarakani kuendelea na muhula wake wa pili.
Moja ya kazi kubwa zinazomsubiri ofisini ni kukabiliana na deni la Taifa linalotajwa kufikia Pauni trilioni 3.3.
Published:


