18 C
New York

Mke wa Gbagbo kugombea urais Ivory Coast

Published:

YAMOUSSOUKRO, Ivory Coast
MKE wa Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, ni miongoni mwa wagombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Simone Gbagbo mwenye umri wa miaka 76, atamvaa Alassane Ouattara (83), ambaye naye ametangaza kuwania urais katika Uchaguzi wa Oktoba, mwaka huu.
Ouattara aliingia madarakani baada ya Simone na mumewe, Gbagbo, kuwekwa chini ya ulinzi wakati wa machafuko ya Uchaguzi wa mwaka 2010.
Ikumbukwe, jina la Gbagbo limeondoshwa kwenye kinyang’anyiro cha urais, kama ilivyo kwa Waziri Mkuu wa zamani, Pascal Affi N’Guessan.
Ouattara alipaswa kuongoza kwa awamu mbili pekee lakini alibadilisha Katiba mwaka 2016 na kujipa uhalali wa kugombea tena.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img