9.2 C
New York

Umoja wa Mataifa waonya uhalifu wa kivita DRC

Published:

KINSHASA, DRC
UMOJA wa Mataifa umezionya pande mbili zinazopigana nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ukisema zinahusika katika uhalifu wa kivita nchini humo.
Licha ya jitihada za kutafuta suluhisho, bado kuna vita inayoendelea kati ya wanajeshi wa Serikali na wapiganaji wa M23.
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa jana imesema umekuwapo ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu wakati huu wa vita.
Kwa mujibu wa ripoti, wapiganaji wa pande zote mbili wamekuwa wakijihusisha na vitendo vichafu, ikiwamo udhalilishaji wa kingono dhidi ya wanawake.
Aidha, ripoti ililaani kitendo cha M23 kuendelea kuajiri na kuwatumia watoto kwenye mapigano hayo.
Vilevile, wanajeshi wa Serikali wameshutumiwa kwa makosa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuua raia wasio na hatia.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img