KINSHASA, DRC
SERIKALI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imetangaza maambukizi mapya ya Ebola na vifo 15 vitokanavyo na ugonjwa huo.
Ikumbukwe, hizi ni taarifa mpya za maambukizi ya Ebola tangu ubonjwa huo uliporipotiwa kuondoka DRC miaka mitatu iliyopita.
Kwa mujibu wa taarifa, maambukizi mapya yameibuka katika Jimbo la Kasai lililoko Mashariki mwa Kinshasa.
Kwa upande wake, Wizara ya Afya ilieleza kuwa taarifa za maambukizi zilianza Agosti 20, mwaka huu baada ya mwanamke mjamzito kufanyiwa vipimo alipokuwa na changamoto ya kutapika na joto kali la mwili.
Katika hatua nyingine, Shirika la Afya la Kimataifa (WHO) limeonya kuwa huenda kiwango cha maambukizi kikaongezeka zaidi.
Aidha, WHO ilieleza mikakati yake ya kukabiliana na ugonjwa huo, ikiwamo kusambaza vifaa vya kujikinga kwa wahudumu wa afya.
DRC imekuwa na historia mbaya na Ebola kwani ugonjwa huo ulisababisha vifo takribani 2,300 kuanzia mwaka 2018 hadi 2020, kwa ujibu wa taarifa ya WHO.
Sehemu ya itihada za WHO katika kuisaidia DRC ni pamoja na msaada wa dozi 2,000 za chanjo ya ugonjwa huo iitwayo ‘Ervebo Ebola’.
Published:


