JERUSALEM, Palestina
SHAMBULIZI la anga lililofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza limemuua Msemaji wa Kundi la Hamas, Abu Obeida.
Taarifa ya kifo chake inakuja baada ya awali jeshi la Israel (IDF) kutangaza kushambulia eneo la al-Rimal walilolitaja kuwa ni makazi ya magaidi.
Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi la Israel alilipongeza jeshi hilo akisema limefanya kazi nzuri katika Ukanda wa Gaza.
Aidha, Waziri huyo, Israel Katz, ametangaza kuwa bado Israel itaendelea kuwapa wakati mgumu wapiganaji wa Hamas.
Hata hivyo, Hamas haijathibitisha kifo cha Obeida, licha ya kukiri kuwapo kwa shambulizi la anga la Israel lililobisha vifo kwa raia.
Ikumbukwe, hotuba ya mwisho ya Obeida ni ile ya Ijumaa ya wiki iliyopita, ambapo aliionya Israel juu ya mpango wake wa kuivamia Gaza.
Published:


