WASHINGTON, Marekani
RAIS wa Palestina, Mahmoud Abbas, amepigwa marufuku kuingia Marekani, hivyo atakosa nafasi ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao mjini New York.
Abbas amekumbana na kizuizi hicho, sambamba na viongozi wengine waandamizi 80 wa Palestina.
Hata hivyo,. hatua ya kuzuiwa kuingia Marekani imewashitua wengi kwa kuwa Taifa hilo ndilo linalogharamia safari za viongozi wa mataifa yote wataohudhuria Mkutano wa UN.
Ikumbukwe, Marekani imekuwa ikiwashutumu kwa madai ya kukwamisha jitihada za kumaliza mgogoro uliopo kati yao na Israel.
Katika hatua nyingine, uamuzi wa Marekani unakuja huku Ufaransa ikiwa imeshatangaza kuiunga mkono Palestina katika harakati zake za kutambulika kama nchi huru.
Kwa upande wake, Abbas ameeleza kusitishwa na uamuzi wa Marekani kumzuia kuingia New York, akisema unapingana na sheria za kimataifa.
Ikumbukwe, Palestina, licha ya kutotambulika kama nchi huru, bado ina tiketi ya kuhudhuria Mkutano wa UN, hivyo Abbas kuzuiwa ni kuinyima haki.
Published:


