Nyota wa zamani wa Simba na Yanga, Emmanuel Okwi, raia wa Uganda amejiunga na Police FC ya Rwanda akitokea AS Kigali ya nchini humo ambayo aliitumikia msimu uliopita na kuibuka mchezaji bora wa klabu wa msimu wa 2024/2025.
Hii inakuwa klabu ya tatu kwa Okwi kuichezea Rwanda, aliwahi pia kukipiga Kiyovu FC ya nchini humo.


