6.4 C
New York

Mataifa yanayoongoza kwa watu wake kuwa ‘singo’

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini
JAPAN inatajwa na tafiti mbalimbali kuwa asilimia 40 ya raia wake hawako kwenye mahusiano ya kimapenzi. Kwamba si tu hawako kwenye ndoa, bali pia wako ‘singo’.
Kama hiyo haitoshi, asilimia 34 ya raia wake wenye umri kati ya miaka 20 hadi 49 wanatajwa na tafiti hizo kutokuwahi kabisa kujihusisha na mapenzi.
Sasa, wakati hali hiyo ikisabaisha kiwango kidogo cha kuzaliana, inatajwa kusababishwa na gharama kubwa za maisha, ‘ubize’ wa kazi, na hisia kwamba mahusiano yanabana uhuru wao.
Miyoko Taniguchi ana umri wa miaka 41 na ni miongoni mwa wanawake wengi nchini Japan wanaofurahia kutokuwa kwenye mahusiano. “Ni raha sana. Ni raha kuliko kuwa na mtu (mapenzi),” anasema.
Licha ya kuwa kinara duniani, Japan si nchi pekee ambayo asilimia kubwa ya raia wake wamegoma kabisa kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi. Korea ya Kusini nayo imo.
Kufikia mwaka 2023, takwimu zilionesha kuwa watu wasio kwenye mahusiano ni asilimia 42 ya raia wa nchi hiyo. Kama ilivyo kwa Japan, sababu ni zile zile, ikiwamo ubize wa kazi na kutaka uhuru.
Kwa upande wa barani Ulaya, Sweden inaingia kwenye mkumbo huo wa raia wake wengi kuamua kuwa singo, badala ya kutafuta wenza. Takwimu za sasa zinaonesha kundi hilo ni asilimia 45 ya raia wa Taifa hilo.
Wakati msisitizo wa walio wengi ukiwa ni elimu na kazi, ndoa na mahusiano ya kimapenzi umebaki kuwa ni utamaduni wa watu wachache nchini Sweden.
Kwamba kipaumbele cha walio wengi ni ustawi wa mtu binafsi, kwa maana ya mafanikio kwenye elimu au kazi, na si kuoa au kuolewa kwa lengo la kutengeneza familia.
“Sijawahi kuona shida ninapoishi bila mpenzi. Nawajua watu wengi, wanaume kwa wanawake, wanaoishi kama mimi,” anasema Andreas Sjoström anayeishi mjini Gothenburg.
Marekani na Ujerumani ni mataifa mengine yanayotajwa kuwa na ongezeko kubwa la raia wake kuchagua kuishi nje ya mahusiano ya kimapenzi. Kwa Ujerumani, asilimia 40 ya raia wake wako singo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img