26.6 C
New York

Slot ashauriwa ‘kumpotezea’ Salah

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza
MKONGWE wa Liverpool, Steve Nicol, anaamini ni wakati sasa kwa kocha Arne Slot kuacha kumpa nafasi staa wa timu hiyo, Mohamed Salah.
Kwa mujibu wa Nicol, kwa sasa Salah si mchezaji anayeweza kutegemewa kikosini, hivyo ni bora Mholanzi huyo akaamua kumwacha benchi.
Nicol ameibuka na madai hayo baada ya Liverpool kutandikwa mabao 3-0 na Manchester City katika mchezo wa wikiendi iliyopita.
Haikuwa kufungwa na Man City tu, bali ni ilikuwa ni mechi ya tano kwa Liverpool kukosa matokeo ya ushindi msimu huu.
Kutokana na mwenendo usioridhisha, mabingwa watetezi hao wa Ligi Kuu wako nafasi ya nane katika msimamo, wakiwa wameachwa pointi nne na Man City inayoshika nafasi ya pili nyuma ya Arsenal.
Salah, kama ilivyo kwa wachezaji wengi wa Liverpool, hajauanza vizuri msimu huu, ambapo amefunga mabao Matano pekee katika mechi 16 za mashindano mbalimbali.
Hata hivyo, kwa upande wa Nicol, kocha Slot anapaswa kuangalia mchezaji mwingine wa kumpa nafasi ya nyota huyo wa kimataifa wa Misri.
“Kwa sasa, jambo pekee unaloweza kufanya ni kumwacha benchi, ajitathimini na kuja na morali mpya,” amesema lejendari huyo wa Anfield.

Related articles

Recent articles