HARARE, Zimbabwe
WAKONGWE wa Ligi Kuu ya soka ya Zimbabwe, Abas Amidu na Reuben Mhlanga, wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Amidu aliyewahi kutamba na CAPS United na Mhlanga aliyekuwa Dynamos, walikamatwa wakiwa kwenye harakati za kusafirisha mzigo huo nje ya nchi.
Taarifa zinaeleza kuwa walinaswa katika Barabara ya Kwekwe-Kadoma wakiwa na kilo 750 za dawa hizo zenye thamani ya Dola za Marekani 75,000.
“Wawili hao walikamatwa wakiwa na kilo 750 kwenye gari la rangi ya fedha aina ya Honda Shuttle lenye namba za usajili AGP 6776…”
Kwa upande mwingine, taarifa ya polisi imeeleza kuwa bado uchunguzi unaendelea juu ya washukiwa.
Published:


