20.3 C
New York

Amorim: Sihofii kufutwa kazi Man United

Published:

MANCHESTER, Uingereza
KOCHA wa Manchester United, Ruben Amorim, amesema tetesi za kufungashiwa virago klabuni hapo hazimuumizi kichwa kwa sasa.
Amorim amekuja na kauli hiyo baada ya kuishuhudia Man United ikitandikwa mabao 3-1 na Brentford katika mchezo wa wikiendi hii.
Kwa matokeo hayo, Man United imekusanya pointi 34 pekee katika mechi 33 za Ligi tangu kocha huyo raia wa Ureno alipoanza kuliongoza benchi la ufundi.
“Sina wasiwasi na kazi yangu. Mimi siyo mtu wa aina hiyo (kuhofia kufukuzwa),” alisema Amorim katika mahojiano yake na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).
Msimu uliopita, kocha huyo wa zamani wa Sporting Lisbon alikuwa kwenye wakati mgumu baada ya Man United kumaliza katika nafasi ya 15 ya msimamo wa Ligi.
“Sio uamuzi wangu (kufutwa kazi) lakini nitapambana tufanye vizuri kwa kila dakika nitakayokuwa hapa,” alisema Amorim.

Related articles

Recent articles