13.9 C
New York

Rais Ufaransa atupwa jela miaka mitano

Published:

PARIS, Ufaransa
RAIS wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani.
Wakati huo huo, adhabu hiyo imeenda sambamba na hatua ya Mahakama Kuu jijini Paris kumtaka Sarkozy alipe faini ya Dola za Marekani 117,000.
Sarkozy ameshukiwa na rungu hilo kwa kile kilichoelezwa kuwa alihusika katika ufisadi wa mamilioni ya fedha aliyopea na aliyekuwa rais wa Libya, hayati Kanali Muammar Gaddafi.
Waendesha mashitaka wamedai kuwa Sarkozy alipewa fedha hizo akimuahidi Gaddafi kuwa angemsaidia kusafisha jina lake mbele ya mataifa ya Ulaya.
Inaelezwa kuwa Sarkozy alijichotea fedha na kisha kuzielekeza katika kampeni zake za kuwania urais mwaka 2007.
Akizungumza baada ya hukumu hiyo, Sarkozy mwenye umri wa miaka 70, ambaye aliiongoza Ufaransa kuanzia mwaka 2007 hadi 2012, alisema atakata rufaa.
Wakati huo huo, mwanasiasa huyo aliikosoa hukumu hiyo akisema ni sehemu ya siasa za kumchafua.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img