22.6 C
New York

Cape Verde bado pointi 3 tu kutinga Kombe la Dunia

Published:

PRAIA, Cape Verde
USHINDI wa nyumbani wa bao 1-0 dhidi ya Cameroon unaifanya timu ya taifa ya Cape Verde iwe kwenye nafasi nzuri ya kufuzu fainali zijazo za Kombe la Dunia.
Kila timu ikiwa imebakiza mechi mbili, ‘Blue Sharks’ sasa wako kileleni mwa Kundi D wakiizidi pointi nne Cameroon inayoshika nafasi ya pili.
Wakiwa nyumbani jana, waliiduwaza na kuimaliza Cameroon kwa bao la dakika ya 54, mfungaji akiwa ni Livramento.
Hivyo, Blue Sharks wanahitaji pointi tatu pekee katika mechi mbili zijazo dhidi ya Libya na Eswatini ili kukata tiketi ya kwenda Kombe la Dunia.
Lakini, huu ni upande mwingine wa maajabu ya Taifa hilo lenye watu wasiozidi 600,000 kwani lilishangaza wengi lilipofika robo fainali ya AFCON mwaka 2013 na 2023.

Related articles

Recent articles