16.1 C
New York

Suarez afungiwa mechi sita Marekani

Published:

MIAMI, Marekani
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Liverpool, Luis Suarez, amefungiwa mechi sita baada ya kitendo chake cha kumtemea mate kocha wa timu pinzani.
Suarez alimfanyia hivyo kocha wa Seattle Sounders baada ya timu yake ya Inter Miami kufungwa mabao 3-0 katika mchezo wa fainali ya Kombe la Ligi.
Ikumbukwe, adhabu hiyo inamkuta staa huyo akiwa tayari anayo ile ya kufungiwa mechi sita za Ligi Kuu.
Kutokana na hilo, mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona ametumia akaunti zake za mitandao ya kijamii kuwaomba radhi mashabiki wa Inter Miami.
Kwa upande mwingine, mchezaji mwenzake, Sergio Busquets, naye amefungiwa mechi mbili baada ya kuonekana akimpiga ngumi kiungo wa Seattle Sounders, Obed Vargas.
Pia, rungu limemkuta kocha wa Sounders, Steven Lenhart, ambaye amefungiwa mechi tano.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img