16.1 C
New York

Weah, Drogba kupinga ubaguzi wa rangi FIFA

Published:

NYON, Uswis
WAKONGWE wa soka, George Weah na Didier Drogba, wameteuliwa kuingia kwenye jopo la wachezaji 16 wa zamani watakaoendesha kampeni ya kupinga vitendo vya ubaguzi wa rangi.
Uteuzi huo umefanywa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na ni sehemu ya utekelezaji wa Azimio la Mkutano Mkuu wa mwaka jana nchini Thailand.
Weah aliyewahi kuituikia AC Milan na Drogba aliyekipiga Chelsea, wanaungana na wakongwe wengine kutoka mataifa 14.
“Soka ni kwa ajili ya umoja na maendeleo. Pia, husaidia kuimarisha ubinadamu,” alisema Weah, raia wa Liberia na mchezaji pekee barani Afrika kuwahi kuibeba tuzo ya Ballon d’Or.
Kwa upande wake, Rais wa FIFA, Gianni Infantino, amesema jopo hilo litakuwa na mchango mkubwa katika vita ya kukabiliana na vitendo vya ubaguzi wa rangi kwenye mchezo wa soka.
“Tuwe wawazi tu, ubaguzi wa rangi, si tu ni vibaya, bali pia ni uhalifu,” alisema Infantino.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img