LOS ANGELES, Marekani
NYOTA wa tenesi raia wa Belarus, Aryna Sabalenka, ametinga hatua ya fainali ya michuano ya US Open inayoendelea nchini Marekani baada ya ushindi dhidi ya Jessica Pegula.
Hii inakuwa mara ya tatu mfululizo kwa Sabalenka kuingia fainali, akifanya hivyo msimu uliopita na kutwaa taji la mashindano hayo.
Katika mchezo wa nusu fainali jana, Sabalenka aliibuka na ushindi wa seti 4-6 6-3 6-4 mbele ya Pegula.
“Ulikuwa ni mchezo mgumu, (Pegula) alicheza kwa kiwango kizuri sana, alijitoa mno na nilipaswa kutumia nguvu kubwa Zaidi ili kupata ushindi,” alisema Sabalenka.
Hivyo basi, sasa anasubiri mshindi kati ya Naomi Osaka na Amanda Anisimova kwa ajili ya mchezo wa fainali unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi hii.
“Naamini naweza kufanya vizuri zaidi. Ushindi wa leo (jana) una maana kubwa. Nitakuja hapa Jumamosi kwa lengo la kupata ushindi tu, nitacheza kama mechi pekee iliyobaki katika maisha yangu ya tenesi,” alisema Sabalenka.
Published:


