9.8 C
New York

Newcastle haipoi, yasajili straika Bundesliga

Published:

LONDON, Uingereza
MATAJIRI wa Newcastle United wameweka rekodi ya usajili wa bei mbaya klabuni hapo kwa kumnasa straika wa Stuttgart, Nick Woltemade.
Hilo ni pigo kubwa kwa Bayern, ambayo ilijaribu kumsajili lakini Stuttgart iligomea ofa zao mbili majira haya ya kiangazi.
Woltemade mwenye urefu wa futi 6 na inchi 6, ametua Newcastle kwa Pauni milioni 69 na ameshasaini mkataba wa miaka sita.
Msimu uliopita, alifunga mabao 17, likiwamo la fainali ya Kombe la Ligi, ambapo Stuttgart walitwaa ubingwa.
Nyota huyo anavunja rekodi ya Alexander Isak, ambaye Newcastle ilitumia Pauni milioni 63 kumng’oa katika klabu ya Real Sociedad miaka mitatu iliyopita.
Usajili wa Woltemade umelenga kuziba pengo la Isak anayeng’ang’ania kujiunga na Liverpool.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img