Utafiti wa TDHS-MIS 2015-16 unaonyesha kuwa 42% ya wanawake wa mijini ni wazito au wanene mara mbili zaidi ya wale wa vijijini.
Uzito uliokithiri na unene kwa wanawake wa Tanzania umeongezeka mara mbili zaidi katika kipindi cha miaka 25 iliyopita, kutoka 11% mwaka 1991-92 mpaka 28% mwaka 2015-16.
Aidha, kwa mujibu wa utafiti wa TDHS-MIS wa mwaka 2015-16 uliohusisha wanawake wenye miaka 15-49 unaonyesha kuwa, mwanamke 1 kati 10 wa Tanzania ni mwembamba sana lakini 28% ya wanawake wanauzito uliokithiri au wanene sana.
Tatizo hilo linaelezwa kuongezeka sambamba na elimu ya utajiri.