13.5 C
New York

Elikia Mbinga: Staa wa Ajax aliyeacha soka kisa muziki

Published:

AMSTERDAM, Uholanzi

AKIWA na umri wa miaka 17, Elikia Mbinga alikuwa na ndoto za kuja kuwa mwanasoka maarufu, wakati huo akicheza katika ‘academy’ ya klabu ya PEC Zwolle ya nchini Uholanzi.

Baada ya kufanya vizuri akiwa na PEC Zwolle, Mbinga alisajiliwa na academy ya Ajaxm ya jijini Amsterdam, ambako huko alikutana na Jurrien Timber, Ryan Gravenberch na Brian Brobbey.

Hata hivyo, licha ya kuwa nahodha wao katika baadhi ya mechi, wenzake hao waliweza ‘kutoboa’ na kuwa wachezaji wakubwa wa Ajax. Mbinga aliishia kurudi zake PEC Zwolle mwaka 2021 akiwa na umri wa miaka 20.

Akiwa na umri wa miaka 25 kwa sasa, Mbinga ameamua kabisa kubadili upepo, ambapo ameachana na soka na kujikita katika muziki.

Lakini, si kwamba imetokea kwa bahati mbaya kuingia kwenye muziki. “Nilikuwa napenda sana muziki. Nilikuwa nafuatilia kila mwanamuziki mpya aliyekuwa anafanya vizuri.

Ni mmoja ya chipukizi wa muziki wa Afrobeat wanaofanya chini Uholanzi, huku nyimbo zake zikifuatiliwa mara zaidi ya milioni 30 kwenye jukwaa la wa Spotify.

“Kwa upange wangu, ilikuwa ni ndoto yangu ya kufanya kitu kwenye muziki, kutengeneza nyimbo zangu mwenyewe.”

Wimbo wake uitwao ‘Mentality’ wa mwaka 2024 umesikilizwa mara milioni 16 kwenye jukwaa hilo. “Kwangu, mafanikio yote kwenye muziki ni kama kufunga mabao au kutoa ‘asisti’ au kucheza vizuri kwenye mechi,” amesema.

Mapema mwezi huu, Mbinga alisafiri hadi Uingereza kuipigia ‘promo’ albamu yake mpya, ‘First of a Kind’, na huko alikutana na washikaji zake, Jurrien na Quinten Timber aliokuwa nao Ajax.

Akiwa huko, Mbinga alikuwa jukwaani kuitazama Arsenal ya Jurrien ilipocheza mechi ya Ligi ya Mabingwa, kisha kwenda kumtazama Quinten anayekipiga Crystal Palace.

Miongoni mwa wanasoka ambao wamekuwa mstari wa mbele kumsapoti kwenye muziki wake ni mshambuliaji wa zamani wa Barcelona anayekipiga katik klabu ya AS Monaco, Ansu Fati.

Ifahamike kuwa Fati na Mbinga wamekuwa marafiki wakubwa tangu walipokutana kwa mara ya kwanza katika michuano ya vijana miaka mingi iliyopita.

Februari, 2026, Mbinga alimtungia wimbo mshikaji wake huyo akimpa moyo kwa changamoto za majeraha na kushuka kiwango tangu alipopata ustaa akiwa na Barceona mwaka 2019.

Related articles

Recent articles