13.5 C
New York

Orlado Pirates yalazimisha sare kwa Simba

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini – DAR

ORLANDO Pirates ya Afrika Kusini imeambulia sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba katika mchezo wa Kundi C msimu huu wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Katika mechi hiyo iliyochezwa leo Novemba 29, 2026 jijini Dar es Salaam, Wekundu wa Msimbazi walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Libasse Gueye aliyezipasia nyavu za Orlando dakika ya 10 tu ya kipindi cha kwanza.

Dalili za Simba kuondoka na ushindi zilionekana tena dakika tatu kabla ya timu hizo kwenda mapumziko baada ya beki Anthony Mligo kuipatia bao la pili.

Hadi dakika 45 zinamalizika na mchezo huo kwenda mapumziko, wenyeji Simba walikuwa mbele kwa mabao hayo ya Gueye na Mligo.

Hata hivyo, Orlando walirudi kipindi cha pili wakiwa na nguvu, ambapo walipata bao la dakika ya 53, mfungaji akiwa ni Tshepang Moremi.

Dakika 10 baadaye, wageni hao kutoka mjini Soweto iliufanya ubao wa matokeo usomeke sare ya mabao 2-2 baada ya Simphiwe Selepe kuzifumania nyavu za Simba.

Ni kwa matokeo hayo, kila timu ina pointi moja, wakati RS Berkane ikiongoza Kundi hilo ikiwa na pointi tatu baada ya kuifunga Colombe Sportive mabao 4–1 katika mchezo wa jana.

Related articles

Recent articles