13.5 C
New York

Mourinho afikisha mechi 197 akiwa Madrid

Published:

MADRID, Hispania

MECHI ya jana dhidi ya Alaves ilikuwa ya 197 kwa Jose Mourinho akiwa kwenye benchi la ufundi la Real Madrid, licha ya kwamba ni kwa awamu mbili tofauti.

Kwa idadi hiyo, Mourinho amemfikia Leo Beenhakker na kuingia kwenye orodha ya makocha walioiongoza Madrid kwenye michezo mingi.

Katika mechi zake hizo, ‘Special One’ ameshinda 144, ametoa sare 28 na kufungwa mara 25 pekee.

Wakati huo huo, Mourinho anakuwa amezidiwa na makocha wanne tu kwa idadi ya michezo mingi, ambao ni Miguel Munoz (605), Carlo Ancelotti (353), Zinedine Zidane (263), na Vicente del Bosque (246).

Mechi 197 za Mourinho zinagawanyika katika michuano mbalimbali, ambayo ni La Liga [128], Ligi ya Mabingwa [41], Copa del Rey [24], na Spanish Super Cup [4].

Related articles

Recent articles