Na Mwandishi Wetu, Gazetini – DAR
HATIMAYE Issa Ali Mangungu amewapiga bao washindani wake wawili na kutangazwa kuwa Rais mpya wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC).
Mangungu amepata ushindi wa kishindo baada ya kukusanya kura 17 kati ya 24 zilizopigwa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo Novemba 24, 2026.
Katika nafasi hiyo, Mangungu alikuwa akishindana na Wakili Stephen Mosha lakini mwenzake huyo aliyeshika nafasi ya pili amepata kura sita, huku Rwegasira Joseph Samson akiambulia moja tu.
Kwa upande mwingine, Fredrick Charles amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais, huku viongoi wengine wakiingia kupitia Kanda.
Viongozi hao ni Bakari Khatibu [Mashariki], Bashir Masangula [Magharibi], Chesi Masanja [Ziwa], Rosemary Masawe [Kaskazini] na Aniset ius Lusale [Kati].
Wakati huo huo, Christina Koroso amepata nafasi ya Mwakilishi wa Wanawake akiwa amejipatia kura 15.


