8.6 C
New York

UN: Ndugu, wenza huua wanawake watano kila dakika 60

Published:

NEW YORK, Marekani

WANAWAKE na wasichana takribani 47,000 huuawa na ndugu au wenza wao kila mwaka, sawa na watano kila baada ya saa moja [Dakika 60].

Hayo yamefichuliwa katika ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa [UN] kwa mwaka 2025, ikieleza kuwa vifo hivyo husababishwa na ndugu au wapenzi wao.

Ripoti hiyo iliyotoka siku chache zilizopita, imetokana na utafiti wa UN katika nchi 122 duniani.

Afrika imeonekana kuwa na kiwango kikubwa zaidi, ambapo wanawake na wasichana 22,100 waliuawa mwaka 2025, ikifuatiwa na Asia [15,100], Marekani [7,400], na Ulaya [2,100].

Katika hatua nyingine, utafiti ulibaini kuwa mmoja kati ya wanawaake watatu duniani amekumbana na vitendo vya unyanyasaji kimwili, mathalan kupigwa, na kingono.

Hata hivyo, licha ya ukubwa wa tatizo hilo, ni asilimia 7 pekee kati yao walioweza kwenda kuripoti katika vituo vya polisi.

Related articles

Recent articles