8.6 C
New York

Mbunge awataka wananchi kujenga nyumba zinazohimili maafa

Published:

Mwandishi Wetu, Gazetini – SHINYANGA

MBUNGE wa Ushetu Emmanuel Cherehani ametoa msaada wa mabati na simenti kwa waathirika wa mvua iliambatana na upepo mkali na kuezua nyumba zaidi ya 40 katika Kata ya Nyankende wilayani Kahama mkoani Shinyanga na kusababisha baadhi familia kukosa makazi,na chakula pamoja na kuharibu vyakula vilivyokuwa vimetunzwa ndani ya nyumba hizo.

Mvua hii imeleta athari katika Kijiji cha Imalabupina katika kata ya Nyakende mkoani Shinyanga ambapo baadhi ya kaya zimeezuliwa mapaa na zingine kubomoka, huku baadhi ya waathirika katika kijiji cha Imalabupina wakikosa makazi na chakula,

“Tunalima pamba, mahindi mpunga na mazao mengine, lakini niwasihi mnapovuma wekezeni kidogo kidogo katika ujenzi wa nyumba zilizo imara, zinazohimili mitikisiko ambazo zitasaidia kuepukana na mdhara kama haya, nimetoa mabati na simenti kwa ajili ya msaada wa haraka haraka wa kuezeka nyumba na kujikinga kwa muda huu,” amesema Cherehani.

Nao baadhi ya wahanga wa tukio hilo kutoka katika kijiji cha Imalabupina wameeleza namna tukio lilivyotokea na kuwasababishia madhara makubwa ikiwa pamoja na kulowanisha vyakula viliyokuwa vimetunzwa ndani,

“Ilikuja mvua ya upepo nyumba zikaezuliwa na nyingine zikabomoka pamoja na magunia ya mpunga yakalowana tumebaki hivihivi,” amesema Rukia Saleh.

“Tulipoteza chakula na hakuna pa kulala, tunaomba msaada kupata mahema kwa ajili ya kujikinga kwa sababu hichi ni kipindi cha mvua na hatuwezi kuisitishwa kwa sababu tuna changamoto, kwa hili tunaomba msaada wa mahema kwa kipindi hiki” amesema Mashaka Charles.

Kwa upande wake Mtendaji kata ya Nyankende, Yusuph Daudi ameeleza namna walivyowasaidia wahanga hao kwa kupata makazi ya muda kutoka kwa jamaa na majirani zao kama msaada wa awali.

Related articles

Recent articles