8.6 C
New York

Nini kimemkuta Viktor Gyokeres?

Published:

LONDON, Uingereza

ARSENAL walimwaga Pauni milioni 64 kumsajili Viktor Gyokeres wakiamini straika huyo wa kimataifa wa Sweden angehamishia mabao yake Emirates baada ya uwezo mkubwa akiwa na Sporting Lisbon.

Gyokeres aliwapa matumaini makubwa mashabiki wa Arsenal baada ya kufunga mabao 21 katika msimu wake wa kwanza, ambao pia timu hiyo ilitwaa taji la Ligi Kuu ya England [EPL].

Safari hii, ukiwa ni msimu wake wa pili Emirates, nyota huyo ameonekana kupotea kwani ameingia mara moja pekee katika kikosi cha kwanza cha Arsenal katika mechi za Ligi Kuu hiyo.

Mbaya zaidi, Gyokeres hajaweza kufunga bao katika mechi zote nane za EPL alizopata nafasi ya kucheza.

Kwa ujumla, mshambuliaji huyo amefunga mabao mawili pekee katika mechi 15 za mashindano mbalimbali [Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa na Carabao Cup].

Related articles

Recent articles