2.3 C
New York

Waasi DRC wadai kuitungua ndege ya jeshi

Published:

KINSHASA, DRC

JESHI la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo [DRC] limesema linaitafuta ndege yake iliyopotea, huku waasi wakidai kuitungua huko Mashariki mwa nchi hiyo.

Awali, jeshi lilieleza kuwa limepoteza mawasiliano na ndege yake ndogo ya mizigo aina ya Cessna 208 kutokana na hali mbaya ya hewa.

Hata hivyo, kundi la waasi la Refoundation of the Nation (FRN) limeeleza kuwa limeiangusha baada ya kubaini kuwa ilitaka kufanya mashambulizi mjini Minembwe katika Jimbo la Kivu Kusini.

Taarifa zinaeleza kuwa watu wanne walikuwamo kwenye ndege hiyo iliyopotea Jumapili ya juzi Novemba 23, 2026.

Miongoni mwa waliokuwamo kwenye usafiri hao ni marubani wawili kutoka Uganda na Afrika Kusini.

Related articles

Recent articles