Na Editha William, Gazetini – KAGERA
TIMU ya soka ya Omukishenye FC imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Muhaj Cup 2026 baada ya ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Kashabo FC.
Mchezo huo wa nusu fainali uliochezwa jana Novemba 24, 2026, ulilazimika kuhamia kwenye mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90 za mchezo.
Ni baada ya matokeo hayo, sasa Omukishenye FC inasubiri mshindi wa nusu fainali ya pili itakayozikutanisha Fanicha FC na Mchikichini FC.
Fanicha FC dhidi ya Mchikichini FC ni mtanange mwingine unaotarajiwa kuwa wa kukata na shoka kutokana na ushindani mkali uliooneshwa na timu hizo kwenye mashindano hayo.
Je, ni Fanicha FC au Mchikichini FC itakayokata tiketi ya kukutana na Omukishenye kwenye hatua ya fainali?


