CAIRO, Misri
MISRI inaendelea kuwa nchi iliyobeba mara nyingi taji la fainali za Mataifa ya Afrika [AFCON], licha ya hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Usuluhishi wa Micheszo [CAF] kuitangaza Segenal kuwa mabingwa wa michuano hiyo ya mwaka 2025.
Katika historia ya mashindano hayo makubwa ya Shirikisho la Soka barani Afrika [CAF], ‘Mafarao’ wametwaa ubingwa mara saba.
Historia inaonesha kuwa Misri iliweza kuwa mabingwa wa mashindano hayo katika miaka ya 1957, 1959, 1986, 1998, 2006, 2008 na 2010.
Katika nafasi ya pili, ni Cameroon iliyotwaa mara tano, ikifanya hivyo katika miaka ya 1984, 1988, 2000, 2002 na 2017.
Wakati huo huo, Ghana iko nafasi ya tatu ikiwa imebeba ubingwa mara nne katika miaka ya 1963, 1965, 1978 na 1982.
Nigeria inafuata ikiwa imetwaa mara tatu [1980, 1994 na 2013], kama zilivyo Ivory Coast [1992, 2015 na 2023].
Senegal, baada ya uamuzi wa CAS, imefikisha mataji mawili ya AFCON [2021 na 2025], sawa na Algeria [1990 na 2019] na DR Congo [1968 na 1974].
Kwa upande wake, Morocco imebaki na moja [1976], kama zilivyo Ethiopia [1962], Sudan [1970], Congo [1972], Afrika Kusini [1996], Tunisia [2004], na Zambia [2012].


