CAIRO, Misri
HATIMAYE ule mzozo umefikia ukomo. Ni baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuhulishi wa Michezo [CAS] kuitangaza timu ya Taifa ya Senegal kuwa mabingwa wa fainali za AFCON za mwaka 2025.
CAS imeivua ubingwa Morocco ikiwa ni baada ya Senegal kupokonywa ubingwa, licha ya kushinda bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa mjini Rabat.
Senegal walipokonywa ubingwa baada ya vurugu walizosababisha wachezaji wake, ikiwamo kutishia kugomea mchezo.
Wakionesha kutokukubaliana penalti waliyopewa Morocco, wachezaji wa ‘Simba wa Teranga’ waliingia kwenye vyumba vya kubadilishia, kabla ya staa wao, Sadio Mane, kuwabembeleza kurudi.
Hilo lilisababisha Senegal kuvuliwa ubingwa, uamuzi huo ambao Shirikisho la Soka la Senegal liliupinga na kukata rufaa CAS, ambako kesi hiyo ilisikilizwa na wajumbe watatu mjini Lausanne, Uswis.


