14.8 C
New York

Moto kiwanda cha pipi waua watatu, wajeruhi 36

Published:

JAKARTA, Indonesia

WATU watatu wamefariki na wengine 36 hawajulikani waliko baada ya moto kuteketeza kiwanda cha pipi huko Magharibi mwa Mji wa Java.

Taarifa zinaeleza kwamba kiwanda hicho kiko Wilaya ya Serang katika Jimbo la Banten, umbali wa kilometa 50 kutoka Mji Mkuu wa Jakarta.

Baada ya moto huo kuibuka jana Novemba 21, 2026, timu ya waokoaji ilifika na kuendesha operesheni ya kutafuta wafanyakazi 60 waliokuwamo kwenye majengo ya kiwanda hicho.

Katika taarifa yake, Shirika la Uokoaji la Indonesia limeeleza kuwa watu 15 wameshaokolewa kufikia leo Jumapili.

Pia, Shirika hilo limeeleza kuwa watu watano waliobahatika kuokolewa wako hospitali wakiendelea na matibabu ya majeraha.

Hata hivyo, mamlaka zimedai kuwa bado hazijabaini chanzo cha moto huo, hivyo zinaendelea na uchunguzi.

Related articles

Recent articles