14.8 C
New York

Barca yakaa kileleni ikiitandika Villarreal

Published:

CATALUNYA, Hispania

BARCELONA imefunga mabao matatu ndani ya dakika 10 na kupata ushindi wa 3-2 dhidi ya Villarreal katika mchezo uliochezwa leo Novemba 22, 2026, kwenye Uwanja wa Spotify Nou Camp.

Matokeo hayo yameifanya Barcelona kukaa kileleni mwa msimamo wa La Liga kwa tofauti ya pointi tatu dhidi ya Real Madrid inayoshika nafasi ya pili.

Villarreal walitangulia kwa mabao mawili ndani ya dakika saba za mwanzo wa mchezo, wafungaji wake wakiwa ni Tajon Buchanan [Dk. 5] na Tani Oluwaseyi [Dk. 7].

Rekodi zinaonesha kuwa hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 1981 kwa Barcelona kuruhusu mabao mawili ndani ya dakika saba tu za kipindi cha kwanza.

Baada ya dakika 23, Barcelona walipata mkwaju wa penalti baada ya Oluwaseyi kumchezea rafu Lamine Yamal ndani ya boksi lakini VAR lakini staa huyo alipiga na kukosa.

Katika dakika ya 57, Barcelona walipata bao moja kupitia kwa Gerard Martin, kisha Fermin Lopez akafunga la pili [Dk. 61], kabla ya beki wa Villarreal, Pau Navarro, kujifunga [Dk. 67].

Kwa upande mwingine, kocha wa Villarreal, Inigo Perez, amefikisha mechi sita bila ushindi mbele ya Barca, akifungwa tano na kuambulia sare moja.

Related articles

Recent articles