14.8 C
New York

Arsenal ya Wanawake hali mbaya England

Published:

LONDON, Uingereza

TIMU ya soka ya Wanawake ya klabu ya Arsenal imeendeleza wimbi la sare katika mechi za nyumbani msimu huu wa Ligi Kuu [WSL].

Katika mechi ya leo Novemba 22, 2026, iliyochezwa Emirates, Arsenal imelazimishwa suluhu [0-0] na wenzao wa jijini London, West Ham United.

Hiyo inakuwa sare ya sita mfululizo kwa vijana hao wa kocha Renee Slegers katika mechi zao za nyumbani kwenye Uwanja huo wa Emirates.

Kwa matokeo hayo, sasa wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi hiyo ya Wanawake, wakiachwa pointi nane na Lionesses inayoshika nafasi ya tatu.

Aidha, kabla ya kuivaa West Ham, tayari Arsenal walikuwa na majeraha ya kufungwa mabao 2-0 na Lyon katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyochezwa Alhamisi ya wiki hii.

Related articles

Recent articles