BOGOTA, Colombia
KIUNGO wa timu ya soka ya Taifa ya Argentina, Leandro Paredes, ameanguka ghafla na kupoteza fahamu wakati akihojiwa na waandishi wa habari.
Tukio hilo lilitokea wakati klabu yake ya Boca Juniors ilipotwaa ubingwa wa michuano ya Copa Sudamericana kwa kuifunga Atletico Mineiro ya Brazil mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa mjini Barranquilla, Colombia.
Taarifa zinaeleza kuwa wakati anahojiwa, Paredes aliyewahi kukipiga PSG alizidiwa na joto kali, hivyo kuanguka na kupoteza fahamu.
Hata hivyo, nyota huyo alizinduka baada ya kupatiwa matibabu, kisha kuwashukuru mashabiki kwa kumsapoti kwa jumbe za kumuombea dua.
Kwa upande wake, kocha wa Boca, Rodolfo Arruabarrena, amesema aligundua mapema kwamba kiungo huyo alikuwa akishindwa kuendana na hali ya joto kali.
Paredes alianzia soka lake katika klabu ya Boca, kabla ya kutimkia Ulaya mwaka 2015 na kuzitumikia AS Roma, Zenit Saint Petersburg na PSG.


