14.8 C
New York

Mourinho ataja kipa bora duniani

Published:

MADRID, Hispania

KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho, amemtaja Thibaut Courtois akisema kwa sasa Mbelgiji huyo ndiye kipa bora zaidi duniani.

Mourinho ameyasema hayo katika mazungumzo yake na waandishi wa habari baada ya Madrid kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Celta Vigo.

Licha ya Courtois kuruhusu bao lililofungwa na Pablo Duran, aliokoa mabao mengi ya wazi kuiwezesha Madrid kuondoka na pointi tatu.

Baada ya dakika 90, Mourinho aliulizwa juu ya kiwango cha kipa wake huyo na kusema: “Thibaut Courtois ndiye kipa bora zaidi duniani. Amekuwa bora kwa miaka mingi.”

Courtois alijiunga na Madrid mwaka 2018 akitokea Ligi Kuu ya England [EPL] alikokuwa akiitumikia matajiri wa Darajani, Chelsea.

Related articles

Recent articles