12.9 C
New York

Mkongwe wa soka avamiwa nyumbani, apigwa mapanga

Published:

LAGOS, Nigeria

ALIYEWAHI kuwa nahodha wa timu ya soka ya Taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’, Segun Odegbami, amevamiwa nyumbani kwake na watu wenye silaha na kujeruhiwa kwa kupigwa mapanga.

Lejendari huyo wa kandanda anaishi mjini Abeokuta, Jimbo la Ogun, ambako ndiko alikokutwa na watu hao wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.

Odegbami [74], alikutwa na mkasa huo saa 8 usiku wa Ijumaa ya wiki hii, huku taarifa zikieleza kuwa waliomvamia ni watu watatu.

Taarifa zinaeleza pia, watu hao waliweza kumfikia chumbani baada ya kumdhibiti mfanyakazi wa ndani, pamoja na dereva wake.

Inaelezwa kuwa watu hao walifika na kumuulizia Odegbami na baada ya mfanyakazi na dereva kudanganya kuwa hayupo, walichezea kichapo, kisha akafuatwa ndani.

Mkongwe huyo alicheza mechi 47 akiwa na uzi wa Super Eagles, ambapo alifunga mabao 22 na alikuwa sehemu ya kikosi wakati timu hiyo inatwaa kwa mara ya kwanza ubingwa wa AFCON mwaka 1980.

Related articles

Recent articles