14.2 C
New York

Koffi Olomide: Maisha ya siasa, alivyokimbia ‘figisu’ za Uchaguzi – [7]

Published:

KINSHASA, DRC

KAMA ilivyo kwa wanamuziki wengi duniani, Koffi naye amewahi mara kadhaa kuonekana kwenye ulingo wa siasa tangu mwaka 1992 alipotumbuiza nchini Gabon alikoalikwa na Rais Omar Bongo Ondimba.

Baadaye, alionekana nchini Jamhuri ya Congo alikokwenda kwenye mikutano ya kampeni za uchaguzi, kisha akaibukia Liberia kumuunga mkono mgombea wa urais, George Weah, katika Uchaguzi wa mwaka 2017.

Mwaka 2020, Koffi alieleza matamanio yake ya kuwa sehemu ya uongozi wa Rais wa DRC, Felix Tshisekedi. Miezi mingi baadaye, alijiunga na Alliance des Forces Democratiques du Congo (AFDC), Chama cha siasa kilichokuwa kikiongozwa na Modeste Bahati Lukwebo.

Februari 9, 2022, Rais Tshisekedi alimteua Koffi kuwa balozi wa utamaduni akimpatia hati ya kusafiria ya kidiplomasia. Akawa mwanamuziki wa tatu wa DRC kuwahi kupewa heshima hiyo baada ya Maitre Gim na Dadju.

Wiki chache baadaye, alikutana na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Urithi, Catherine Kathungu Furaha, kujadili mikakati ya Wizara katika kupaisha utamaduni wa DRC nje ya mipaka ya nchi hiyo.

Mwaka 2024, Koffi alitangaza nia ya kugombea nafasi ya seneta katika Jimbo la Sud-Ubangi lakini alijitoa baadaye kwa kile alichodai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na ‘figisu’ nyingi.

Baada ya hapo, Oktoba 19, 2025, alionekana mjini Abidjan kumsapoti mwanasiasa mkongwe aliyekuwa akigombea kiti cha urais, Alassane Ouattara.

Wiki chache baadaye, Chama chake cha AFDC kilimteua Koffi, sambamba na wanamuziki wengine wawili, Werrason na Felix Wazekwa, kuwa sehemu ya washauri wa sera.

Itaendelea …

Related articles

Recent articles