11.8 C
New York

Hizi hapa sita zilizokata tiketi AFCON 2027

Published:

CAIRO, Misri

USIKU wa jana Novemba 17, 2026, timu za soka za taifa za Senegal na Morocco zilifuzu kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika za mwakani [AFCON 2027].

Senegal ‘Teranga Lions’ wamefuzu wakiwa na pointi 10, licha ya kwamba bado wana mechi zao mbili mkononi.

Kwa upande wao, Morocco walikata tiketi kushiriki AFCON 2027 baada ya ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Niger.

Katika mchezo huo Morocco ‘Simba wa Atlas’ walipata bao pekee hilo la mchezo kupitia kwa Abdellah Ouazane aliyeingia kambani dakika ya 22.

Hivyo, Senegal na Morocco zinaungana na Benin, kama ilivyo kwa wenyeji watatu – Kenya, Uganda na Tanzania – kujihakikishia ushiriki wao kwenye AFCON 2027.

Related articles

Recent articles