8.4 C
New York

Xavi afunguka wakitandikwa ‘5G’ na Ujerumani

Published:

AMSTERDAM, Uholanzi

KOCHA wa timu ya soka ya Taifa ya Uholanzi, Xavi Hernandez, amesema vijana wake walikosa upambanaji, hivyo kujikuta wakitandikwa mabao 5-0 na Ujerumani katika mechi ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya [UEFA Nations League] iliyochezwa jana Novemba 16, 2026.

Uholanzi waliangukiwa na mvua hiyo ya mabao, licha ya kwenda mapumziko wakiwa wameruhusu bao 1-0 mbele ya mabingwa hao wa zamani wa Kombe la Dunia.

Kichapo hicho kimekuja zikiwa ni siku chache tu tangu Uholanzi iliposherehekea ushindi mnono wa mabao 7-0 katika mechi yao dhidi ya Ugiriki.

“Siku zote nimekuwa muwazi kwa wachezaji. Najaribu kuelewa kilichotokea lakini nashindwa. Siku tatu zilizopita, tulicheza kwa kiwango bora sana [dhidi ya Ugiriki] na tulionesha daraja tunalolitaka. Leo [jana] imekuwa tofauti,” amesema.

Xavi, kiungo wa zamani wa Barcelona na timu ya Taifa ya Hispania, aliajiriwa kuinoa Uholanzi wiki chache zilizopita akichukua nafasi ya kocha mzawa, Ronald Koeman.

Related articles

Recent articles