13.1 C
New York

Lukaku astaafu soka la kimataifa

Published:

LONDON, Uingereza

MPACHIKAJI mabao wa zamani wa Chelsea, Romelu Lukaku, ametangaza kustaafu timu ya taifa baada ya kuitumikia Ubelgiji kwa miaka 16.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 33, ambaye kwa sasa anakipiga Fenerbahce ya Ligi Kuu nchini Uturuki, ametangaza uamuzi wake huo kupitia akaunti yake ya Instagram.

Lukaku amekuja na hatua hiyo siku moja tu baada ya kuishuhudia Ubelgiji kuifunga Italia na kutinga robo fainali ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya [Nations League].

Katika mchezo huo uliochezwa Ubelgiji na wenyeji kushinda mabao 4-1, alimaliza dakika zote 90 akiwa kwenye benchi la wachezaji wa akiba.

“Kwa kipindi cha miaka 16, nilijitoa kwa kila kitu kwa ajili ya timu ya taifa …” amesema Lukaku akisisitiza kuwa hajutii uamuzi wake wa kustaafu kuitumikia timu hiyo.

Straika huyo anaiacha Ubelgiji akiwa na kumbukumbu ya kuiwezesha kushika nafasi ya tatu katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018 zilizofanyika nchini Urusi.

Katika ngazi ya klabu, Lukaku aliwahi kutamba Ligi Kuu ya England akiwa na klabu za Everton, Manchester United na Chelsea.

Related articles

Recent articles