CAIRO, Misri
TIMU mbili zimeshatolewa katika kinyang’anyiro cha kusaka tiketi ya kushiriki fainali zijazo za Mataifa ya Afrika [AFCON 2027].
Michuano hiyo ya Shirikisho la Soka la Afrika [CAF] itafanyika kwa pamoja katika nchi Jirani tatu za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati; Tanzania, Kenya na Uganda.
Kufikia hatua hii ya mechi za kufuzu, timu zilizokwishaaga ni Somalia na Jamhuri ya Afrika ya Kati [CAR].
Somalia imeaga baada ya kufungwa bao 1-0 na Ghana, mfungaji akiwa ni nahodha wa kikosi, Jordan Ayew, aliyepachika kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 37.
Kwa matokeo hayo, Somalia ‘Ocean Stars’ wamepoteza mechi zote nne za kufuzu za Kundi C, kama ilivyo CAR iliyoko Kundi F.


