8.4 C
New York

Messi aitiwa kazi ya ukocha Argentina

Published:

BUENOS AIRES, Argentina

KOCHA wa timu ya soka ya Taifa ya Argentina, Lionel Scaloni, amemfungulia mlango wa kuwa msaidizi wake nahodha wa zamani wa kikosi hicho, Lionel Messi.

Kwa mujibu wa Scaloni, Messi anakaribishwa muda wowote kwenye benchi la ufundi baada ya kocha msaidizi, Walter Samuel, kuondoka hivi karibuni.

Samuel, ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Argentina kama ilivyo Messi, ameamua kuanza safari ya maisha ya ukocha nje ya kuwa msaidizi.

Akizungumza kuelekea mechi yao ya kesho Novemba 18, 2026, dhidi ya Costa Rica, Scaloni amesema: “Messi alishasema hatocheza tena timu ya taifa. Kama anataka kuja [kama kocha], hakuna tatizo kabisa. Walter Samuel ameondoka, hivyo aje tu.”

Messi alitangaza kustaafu majukumu ya timu ya taifa miezi michache iliyopita na sasa ameendelea kuitumikia klabu yake ya Inter Miami ya Ligi Kuu nchini Marekani [MLS].

Siku chache zilizopita, mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona na PSG aliandika historia mpya MLS baada ya kuwa mchezaji pekee kutwaa mara mbili mfululizo tuzo ya Mfungaji Bora wa msimu.

Related articles

Recent articles