15.7 C
New York

Montana: Usikimbilie kuitwa baba kama huna pesa

Published:

LOS ANGELES, Marekani

RAPA maarufu nchini Marekani, Karim Kharbouch, akifahamika zaidi kwa jina la French Montana, amesema pesa inapaswa kutangulia kabla ya kutafuta Watoto au kuanzisha familia.

Akiojiwa jijini London, Montana aliyeimba ‘Unforgettable’ amesema kuitwa baba ni mzigo unaohitaji mtu anayejimudu kiuchumi.

Montana ni baba mtoto mmoja katika ndoa yake ya zamani na mrembo Deen Kharbouch na kwa sasa mpenzi wake ambaye ni binti wa mfalme wa Dubai ni mjamzito.

Katika ushauri wake, amewahimiza vijana kujitafuta kwanza na kujiweka vizuri kiuchumi, kisha ndipo wafikirie kuhusu kupata Watoto.

“Somo kubwa nililojifunza ni kwamba ukiwa baba utagharamia vitu vingi; chakula, ada ya shule, na mambo mengine.

“Kama huna pesa, ni bora usiwe na mtoto. Ni bora ukasubiri hadi pale utakapokuwa sawa kiuchumi,” amesema.

Related articles

Recent articles