10.5 C
New York

Mke amfukuzisha kazi kocha Misri

Published:

CAIRO, Misri

CHAMA cha Soka cha Misri (EFA) kimetangaza kumvunjia mkataba kocha wa timu ya Taifa hilo, Hossam Hassan, huku kikieleza sababu za kifamilia, hasa mkewe, ndiyo chanzo cha uamuzi huo.

Agosti, 2026, ulitokea ugomvi wa kushikana kati ya wake wawili wa kocha huyo, Howaida Al-Gharbawy na Dina Mostafa wakiwa kwenye hoteli moja nchini Misri.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, Hossam alianguka na kupoteza fahamu wakati akijaribu kuamulia ugomvi huo.

Siku chache baada ya hicho kilichotokea, straika huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Misri alimtwanga talaka mke mkubwa, Howaida, ambaye alikuwa amedumu naye kwa miaka 30.

Miezi michache baadaye, mke mdogo, Dina, naye alianzisha varangati na kutangaza kufungua kesi mahakamani kudai talaka yake.

Tangu hapo, umekuwapo mvutano na majibizano makali kati ya Hossam na bibiye huyo, jambo lililoifanya EFA kuona ni bora kocha huyo akapumzika kwenye majukumu ya timu ya taifa.

EFA wameeleza katika taarifa yao kwamba kinachoendelea kati ya Hossam na mkewe huyo wa zamani kinachafua taswira ya timu ya Taifa ya Misri.

Baada ya kumfuta kazi, Ali Maher anayeinoa klabu ya Ceramica Cleopatra ndiye aliyekabidhiwa mikoba ya kuinoa Misri.

Maher mwenye umri wa miaka 52, ataanza kazi kabla ya Misri kuivaa Malawi [Novemba 13, 2026] katika mchezo wa kuwania tiketi ya kushiriki fainali zijazo za Mataifa ya Afrika [AFCON 2027].

Hossam alianza kuinoa Misri mwaka 2024 na miezi michache tu iliyopita aliiwezesha timu hiyo kuandika historia ya kufika kwa mara ya kwanza hatua ya 16 Bora ya Kombe la Dunia.

Nje ya uwanja, pia kocha huyo amekuwa na mikasa yake ya hapa na pale, ikiwamo kufungiwa mechi tatu na FIFA baada ya kauli zake za kumkosoa mwamuzi wa mechi yao ya Kombe la Dunia dhidi ya Argentina.

Hivi karibuni, alikosolewa vikali na mashabiki kwa kitendo chake cha kumtoa katika dakika ya 60 staa wao, Mohamed Salah, kwenye mchezo waliolazimishwa suluhu [0-0] na Angola.

Ni baada ya hapo, Salah anayekipiga Trabzonspor ya Uturuki aliondoka moja kwa moja kwenye kambi ya timu ya taifa, ikielezwa kuwa hakutaka tena kucheza kwenye viwanja vya nyasi bandia.

Hata hivyo, anaondoka na rekodi nzuri kwani katika mechi 38 alizokaa kwenye benchi la ufundi, Misri imeshinda 21, imetoa sare 10 na kufungwa saba pekee.

Related articles

Recent articles